Mwenye kujibu. Rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad, Familia yake na Swahaba wake wote.
Mwenyekiti na wajumbe wa Mahakama Kuu:
Dr. Swaleh bin Abdurahmani Muhaymid- Mjumbe.
Suleiman bin Abdurahman Al-samhan- Mjumbe.
Hamad Turky Al-muqbil – Mjumbe.
Ahmad bin Abdurahman Al-ba’adiy–Mjumbe.
Abdul-aziz bin Swaleh Al-humeyd.-Mjumbe
Shafi bin Dhafir Al-haqbaaniy. -Mjumbe.
Suleyman bin Hamad Al-muusa. -Mjumbe
Nasir bin Ibrahim Al-habib.-Mjumbe
Ghayhab bin Muhamad Ghayhab.-Mjumbe
Abdurahman bin Abdulaziz Al-kulliyah.-Rais wa Mahakama Kuu.
Gazeti la Wiaam lilifanikiwa kujua kuwepo kwa kamati sita rasmi za kisheria zilizotumwa sehemu kadhaa za Saudi Arabia zikiwa zimepewa dhamana ya kufuatilia mwandamo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kupiga kambi kwenye maeneo maalumu katika maeneo ya Saudi Arabia. Kamati sita hizo zimepangwa katika miji ya Riyadh, Bureydah, Tabuk, Hail, Dammam na Sudeir. Katika kamati hizo, kuna wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Taasisi ya Mfalme Abdulaziz ya Sayansi na Teknolojia, Mahakama ya Mkoa husika pamoja na idadi kadhaa ya wanazuoni na wataalamu wa elimu ya sayari wanaongalia mwezi kwa kujitolea
Maamuzi na: 36/H ya tarehe 29/8/12-1/9/1433H
Tafsiri hii ni kwa hisani ya: Baraza Kuu La Jumuiya Za Answaru Sunna Tanzania (BASUTA)
Barazasunna@gmail.com
Kingdom of Saudi Arabia
Al-jiwaa Riyadh
Mahakama Kuu (ya Saudi Arabia) imetoa tangazo kwamba kesho Ijumaa sawa na 20/7/2012AD itakuwa awali ya siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi, Mahakama Kuu ilifanya kikao kwenye ofisi yake ya kipindi cha kiangazi katika Mkoa wa Taif, kikao kilichofanyika jioni ya Alhamisi, tarehe 29 ya mwezi wa Shaabani 1433H, ili kupitia taarifa zilizoifikia mahakama hiyo kutoka mahakama mbali mbali kuhusu mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wa mwaka 1433H. Na baada ya kuangalia taarifa zote zilizoifikia Mahaka Kuu kuhusu suala hili na kuzitafiti, na kwa kuzingatia maamuzi yake Na: 35/H ya tarehe 3/8/1433H yanayohusu kuthibiti kuingia kwa mwezi wa Shaabani siku ya Alhamisi sawa na 1/8/1433H kwa mujibu wa kalenda ya Ummul-quraa, Mahakama kuu imetoa maamuzi yafuatayo:
Maamuzi namba 36/H ya tarehe 29/8– 1/9/1433H
Kila sifa njema anazistahiki Mwenyezi Mungu pekee. Ama baada ya hayo, imethibiti kwa Mahakama Kuu kuonekana kwa mwezi muandamo wa Ramadhani ya mwaka 1433H jioni ya leo Alhamisi, tarehe ishirini na tisa ya mwezi wa Shaabani, sawa na tarehe kumi na tisa ya mwezi Julai, mwaka 2012 kwa ushahidi mashahidi kadhaa waadilifu, na kwa kuzingatia matamshi sahihi ya Mtume, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, kwamba amesema kuwa: "Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake". Kwa maana hiyo, siku ya kesho Ijumaa sawa na tarehe ishirini ya mwezi Julai, 2012 ndiyo mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka 1433H.
Na Mahakama Kuu wakati inampongeza Mheshimiwa Mtumishi wa Misikiti Miwili Mitukufu, Mheshimiwa Mrithi wa Ufalme, Serikali na wananchi wa Saudi Arabia, wakaazi Waislamu nchini humo na uma wote wa Kiislamu kwa kuingia kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani , inamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwenye uwezo Mkubwa awasaidie Waislamu waweze kufunga, kusimama katika kisimamo cha sala na awakubalie hayo, awafanye wawe wamoja, kauli yao iwe moja, wawe na mahusiano mazuri, ainusuru dini yake, neno lake alifanye liwe juu, Yeye ni Mwenye kusikia, Yuko karibu,
Do'stlaringiz bilan baham: |