هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ”Je, wanangojea (nini) isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli
vya mawingu pamoja na Malaika, na itolewe hukumu? Na kwa Allaah hurudishwa mambo.”(02:210)
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ”Je, wanangojea jingine (lolote) isipokuwa wawafikie
Malaika (kuwatoa roho) au awafikie Mola wako au ziwajie baadhi za Aayah za Mola wako (alama za Qiyaamah kubwa)?”(06:158)
”Allaah Amekwishasikia kauli ya yule (mwanamke) anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Samiy’um-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima - Mwenye kuona yote daima).”(58:01)
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ”Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.”(03:181)
أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ ”Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.”(43:80)
إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ
”Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”(20:46)